NICTBB KUUNGANISHA NCHI ZA EAC NA SADC

 

NICTBB KUUNGANISHA NCHI ZA EAC NA SADC

NICTBB KUUNGANISHA NCHI ZA EAC NA SADC

DAR ES SALAAAM
Mkongo wa Taifa wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (NICTBB) umefikia hatua kubwa katika kukuza mawasiliano ya kikanda, kuunganisha nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kupitia huduma zake.
Hayo yamebainishwa wakati wa hafla ya utiaji saini kati ya Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Mfumo wa Mkongo wa Burundi (BBS) kwa makubaliano mapya ya miaka mitano ijayo ya biashara ya huduma.
Mkataba mpya kati ya TTCL  na BBS, wenye thamani ya shilingi bilioni 8.3  unalenga kuimarisha ushirikiano katika sekta ya mawasiliano kati ya Tanzania na Burundi  na utaendeleza mifumo ya mawasiliano katika eneo la Manyovu kwa Tanzania, maeneo ya Kabanga na Kobelo kwa wananchi wa Burundi.