UMEPITWA FAHAMU MCHANGO WA SEKTA YA KILIMO KWENYE MAENDELEO NCHINI
DAR ES SALAAM
Sekta ya Kilimo nchini inachangia Pato la taifa (GDP) kwa asilimia 26 kwa mwaka na inatoa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa zaidi ya asilimia 62. Sekta hii inakuwa kwa asilimia 4.5 na huchangia mapato yatokanayo na mauzo nje kwa takribani Dola za kamarekani bilioni 2.33 (sawa na shilingi tilioni 5.825 kwa mwaka na pia huchangia asilimia 65 ya malighafi za viwanda, na asilimia 100 ya usalama wa chakula na lishe nchini, ongezeko la mauzo ya nje limekua kutoka shilingi trilioni 5.3 mwaka 2020/2021 hadi shilingi trilioni 5.825 mwaka 2022/23 sawa na ongezeko la 9%
Pia serikali ya awamu ya sita imefanikisha kutoa mbolea ya ruzuku kwa wakulima, mpango ambao umeleta mafanikio makubwa na kuwafaikia wakulima wapatao,074,663
Aidha serikali imefanikisha kuongeza uzalishaji wa mbegu bora kwa 60% kutoka tani 35,199 mwaka 2021/22 hadi tani 44,344 mwaka 2022/23 kutokana na ongezeko la bajeti kutoka bilioni 7.39 mwaka 2021/22 hadi bilioni 43.03 mwaka 2023/24 sambamba na kuongezeka kwa bajeti ya utafiti kutoka bilioni 9.4 hadi bilioni 40.73 mwaka Tani 2023/2024.
