TSH BIL 7.6 KUJENGA IJC NJOMBE
NJOMBE
Serikali kupitia Mahakama ya Tanzania imeidhinisha kiasi cha shilingi bilioni 7.6 kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (Integrated Justice Centre’ -IJC) kinachojengwa mkoani Njombe
Ujenzi wa kituo hicho umezingatia mahitaji mbalimbali yanayoendana na uhalisia na matarajio ya wananchi watakaopata huduma za haki ndani ya jengo hilo Kwa kupunguza gharama za uendeshaji wa mashauri, kuokoa muda na kuongeza uwazi na uwajibikaji kwa watoa haki
Aidha miundombinu hiyo inayojengwa inakwenda sambamba na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia Duniani hasa katika eneo la utoaji haki ikiwa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa IJC Njombe.
