TSH BIL 1.7 KUWAPATIA MAJI VIJIJI VINNE IRINGA
IRINGA
Serikali imepelekea jumla ya shilingi bilioni 1.7 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji katika vijiji vya Itagutwa, Nyabula, Mlanda na Masaka wilayani na Mkoani Iringa ili kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama unaimarika na kuwaondolea wananchi hao adha ambayo walikuwa wanakumbana nayo kwa muda mrefu huku wanawake wakitumia saa kadhaa kila siku kutafuta maji kutoka vyanzo vya mbali, vingi vikiwa vichafu na visababishi vya magonjwa huku vikupunguza fursa za ukuaji wa uchumi.
Mradi huo unatokana na ujenzi wa bwawa la Masaka lililojengwa serikali kupitia Bodi ya Maji Bonde la Rufiji (RBWB).
Bwawa la Masaka lina urefu wa zaidi ya kilometa 1.5 litawawezesha wananchi wa Masaka kupata miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji, mabirika ya kunyweshea mifugo na maji safi na salama.
Nao mradi wa Nyabula-Mlanda una uwezo wa kuzalisha lita 360,000 za maji huku mahitaji ya watu zaidi ya 17,800 wa vijiji hivyo vya Nyabula na Mlanda ikiwa ni lita 150,000.
Aidha Katika kijiji cha Itagutwa zoezi la ulazaji mabomba wa umbali wa kilometa 12.75 , unaendelea ,Ujenzi wa vituo 11 vya kuchotea maji pamoja na ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 75,000.
Utekelezaji wa miradi hiyo ni tiba ya utatuzi wa changamoto za upatikanaji wa maji katika vijiji hivyo na baadhi ya vitongoji kwenye vijiji jirani.
USISAHAU:-Mhe Rais Dkt Samia anayo dhamira yake ya kutunza mazingira na kumtua mama ndoo kichwani.
