TSH TRIL 1.1 ZATUMIKA UJENZI VIWANJA VYA NDEGE
MWANZA
Seriali ya awamu ya sita katika kipindi cha miaka mitatuya uongoz wa Dkt Samia imetumia zaidi ya shilingi trilioni 1.1 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege katika maeneo mbalimbali nchini.
Katika kuendeleza mpango huo, serikali hivi karibuni imetia saini mkataba kati ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na Taifa Mining and Civil Limited wenye thamani ya shilingi bilioni 29 kwa ajili ya kukamilisha mradi wa jengo la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Mwanza.
Mradi mwingine ni ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato unaotekelezwa kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza inatekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 165.62 na awamu ya pili itagharimu shilingi bilioni 194.403.
Miradi mingine ni pamoja na Musoma bilioni 36.638 hadi sasa, uwanja wa ndege wa Shinyanga (49bn/-) Tabora (27bn/-), Sumbawanga (50.9bn/-) na Kigoma (38.63bn/-). Vingine ni kiwanja cha ndege cha Iringa (63.73bn/-), Songwe (28.87bn/-), Songea 37.09bn/-, Mtwara (56.99bn/-), Dodoma (10bn/-) pamoja na Arusha (30bn/=).
