TSH MIL 200 KUUNGANISHA NANYAMBA -MBEMBALEO

 

TSH MIL 200 KUUNGANISHA NANYAMBA -MBEMBALEO

TSH MIL 200 KUUNGANISHA NANYAMBA -MBEMBALEO

MTWARA
Serikali ya awamu ya sita imetoa kiasi cha shilingi milioni 200 kwa ajili ya marekebisho ya barabara kwa kiwango cha lami kuanzia Halmashauri ya Mji Nanyamba (mahakamani) kuelekea vijiji vya Mwang'anga na Mbembaleo vilivyopo katika Halmashauri ya Mji Nanyamba Mkoani Mtwara.
Kiasi hicho cha fedha kimetolewa baada ya kalvati lililopo kati ya Shule ya Msingi Namkuku na Mahakamani kuelekea kata ya Mbembaleo kuharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika Halmashauri hiyo ya Mji Nanyamba.
Kukamilika kwa ukarabati wa kalvati hilo kutawaunganisha tena wananchi wa Nanyamba,Magomeni,Mwang'anga, Mbembaleo kuelekea  Kiyanga na Kitaya na kuwarahisishia kuendelea na shughuli zao za Maendeleo na ujenzi wa Taifa.