DKT SAMIA MGENI RASMI UZINDUZI CEAT

 

DKT SAMIA MGENI RASMI UZINDUZI CEAT

DKT SAMIA MGENI RASMI UZINDUZI CEAT

DAR ES SALAAM.
Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Umoja wa Kampuni za Kichina (CEAT) nchini Tanzania mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza Rais wa Umoja huo Shi Yong, amesema kuwa umoja huo ni muunganiko wa kampuni 72 za Kichina ambayo yanayofanya kazi hapa nchini katika sekta mbalimbali.
Rais huyo amezitaja sekta hizo kuwa ni kwenye miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara, ikiwemo mwendokasi awamu ya 2 na ya 3, madaraja (Wami), viwanja vya ndege (Iringa), miundombinu ya maji (Kidunda mkoani Morogoro), upanuzi wa Bandari za Tanga, Dar es Salaam na ya uvuvi ya Kilwa.
Miradi mingine ipo kwenye sekta ya uchimbaji madini, kilimo ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji.
Yong amesema kuwa kuanzishwa kwa umoja huo utasaidia sana kuwa jukwaa ambalo litakuwa likitumika katika kujadiliana mambo mbalimbali ikiwemo utendaji wa kazi kwa makumpuni hayo yanayofanya kazi hapa nchini.
Kuanzishwa kwa umoja huo ni kielelezo cha ushirikiano wa muda mrefu wa kirafiki kati ya hayati Rais Mao Tse Tung wa Jamhuri ya Watu wa China na hayati Rais Julius Nyerere wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa taarifa zaidi endelea kutufuatilia kwenye mitandao yetu ya kijamii
https://www.bimkubwa.blogspot.com
Twitter (X) :-Bimkubwatanzania
Instagram:-bimkubwatanzania
Facebook:- Bi Mkubwa Tanzania 
Youtube:- bimkubwatanzania