BOTI 2 MPYA KUDHIBITI UVUVI HARAMU ZIWA VICTORIA

 

BOTI 2 MPYA KUDHIBITI UVUVI HARAMU ZIWA VICTORIA

BOTI 2 MPYA KUDHIBITI UVUVI HARAMU ZIWA VICTORIA

MWANZA

Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekabidhiwa boti mbili kutoka Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kufanya doria na kudhibiti uvuvi haramu ndani ya Ziwa Victoria.
Akikabidhiwa boti hizo pamoja na injini tatu na redio maalum kwa ajili ya mawasiliano jijini Mwanza, Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi kutoka katika wizara hiyo Prof. Mohammed Sheikh amesema vifaa hivyo vitasaidia katika juhudi za serikali kulinda, kuendeleza na kukuza rasilimali za uvuvi ndani ya Ziwa Victoria na Tanzania kwa ujumla.
Tanzania kukabidhiwa boti mbili zenye thamani ya takriban Sh Milioni 100 pamoja na vifaa vingine kwa ajili ya doria ndani ya Ziwa Victoria ni mradi uliopita kwenye Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo jumla ya boti sita na injini tisa zimegaiwa kwa nchi tatu za Tanzania, Kenya na Uganda.
USISAHAU:Lengo la serikali ni kuhakikisha inalinda rasilimali za uvuvi , hii ndio maana Mhe Rais Dkt Samia, Januari 30 mwaka huu, aligawa boti za uvuvi za kisasa 55 kati ya 160, lengo likiwa ni kuwawezesha wavuvi kuwa na vifaa bora kwa ajili ya uvuvi ndani ya Ziwa Victoria.