TSH BIL 92 KUZIUNGANISHA KARAGWE-BURIGI - CHATO NA EAC

 

TSH BIL 92 KUZIUNGANISHA KARAGWE-BURIGI - CHATO NA EAC

TSH BIL 92 KUZIUNGANISHA KARAGWE-BURIGI - CHATO NA EAC

KAGERA
Barabara ya kimkakati ya Karagwe kupitia Hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato kilometa 60 inayotegemewa kwa usafirishaji wa mizigo katika nchi za Afrika Mashariki inatarajiwa kukamilika Novemba mwaka huu ambapo serikali imetoa kaisi cha shilingi bilioni 92 kwa ajili ya ujenzi huu na hadi sasa umefikia 33% ya utekelezaji.
Mradi huo unatekelezwa na mkandarasi wa China Road And Bridge Corporation kutoka China, pia kuelekea utekelezaji wake Serikali imetumia kiasi cha shilingi bilioni 2.7 kulipa fidia kwa wananchi zaidi ya 600.
Kukamilika kwa mradi huo, licha ya kutegemewa sana na nchi za Afrika Mashariki  katika masuala ya usafirishaji bado  barabara hiyo itatumika katika shughuli za utalii na kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja katika Wilaya ya Karagwe.