TSH BIL 9.5 ZAWAPA UMEME WANGING’OMBE

 

TSH BIL 9.5  ZAWAPA UMEME WANGING’OMBE

TSH BIL 9.5  ZAWAPA UMEME WANGING’OMBE 

NJOMBE
Kiasi cha shilingi bilioni 9.8 zimetumika kufikisha umeme katika vijiji vyote 108 vya Wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe ikiwa ni mpango wa serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Taarifa  ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini kutoka REA, inaeleza kwamba kwa sasa REA inatekeleza jumla ya miradi mitatu katika maeneo tofauti ya Wilaya ya Wanging’ombe ambayo ni REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili, Mradi wa Ujazilizi Fungu la Pili B pamoja na Mradi wa kupeleka umeme kwenye Vituo vya Afya na Pampu za Maji.
Jumla ya vijiji 361 kati ya 381 vimekwishafikishiwa umeme wa REA Mkoa wa Njombe, sawa na 94.75%