TANZANIA NA MSUMBIJI KUUNGANISHWA KWA DARAJA LA ZEGE

 

TANZANIA NA MSUMBIJI  KUUNGANISHWA KWA DARAJA LA ZEGE

TANZANIA NA MSUMBIJI  KUUNGANISHWA KWA DARAJA LA ZEGE 

RUVUMA
Serikali ipo katika hatua za mwisho ya kusaini mkataba na kumtangaza Mkandarasi atakayejenga barabara ya Likuyufusi - Mkenda (km 122) sehemu ya kwanza Likuyufusi - Mkayukayu (km 60) kwa kiwango cha lami kwa ajili ya kurahisisha biashara ya mazao.
Ujenzi wa barabara hiyo utaenda sambamba na ujenzi wa Daraja la Kisasa la Zege mpakani mwa Tanzania na nchi jirani ya Msumbiji eneo la Mkenda Wilayani Songea kwa ajili ya kuufungua Mkoa wa Ruvuma kiuchumi.
FAIDA:- Kujengwa kwa barabara hii kutawasaidia wananchi wa Mkoa wa Ruvuma ambao ni wazalishaji wakubwa wa mazao na utainua uchumi wa Nchi yetu kuweza kusafirisha kutoka Tanzania kwenda nchi jirani ya Msumbiji.