TSH BIL 73.6 ZATEKELEZA MIRADI YA HEET, SUA

 

TSH BIL 73.6 ZATEKELEZA  MIRADI YA HEET,  SUA

TSH BIL 73.6 ZATEKELEZA  MIRADI YA HEET,  SUA 

MOROGORO
Serikali ya awamu ya sita imekipatia chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)  kiasi cha bilioni 73.6 kwa ajili ya Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) kwa kipindi cha miaka mitatau ya uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassan.
Utekelezaji wa mradi huo ni wa muda wa miaka mitano, 2021/ 2022 na unatarajia kumalizikia kwa mwaka 2025 /2026, lengo lake ni kuongeza udahili wa wanafunzi na kuboresha ubora wa elimu ya juu nchini.
Aidha kati ya fedha wazizotengewa(SUA) Shilingi bilioni 50 ni kwa ajili ya upanuzi wa miundombinu Kampasi za Morogoro ambazo ni Solomon Mahlangu na kampasi kuu ya Edward Moringe, na kiasi cha Sh bilioni 20 zitatumika kwenye upanuzi wa kampasi ya Mizengo Pinda , iliyopo mkoani Katavi ambapo fedha hizo pia zitatumika kujenga majengo ya ufundishaji matatu ambayo yatajengwa mkoani Katavi , Kampasi ya Solomon Mahlangu na jingine kampasi kuu ya Edward Moringe mkoani Morogoro, kujenga jengo la dahalia ( Kaftelia) mkoani Katavi,ujenzi mkubwa na upanuzi wa karakana za mafunzo mbalimbali ambazo zilizopo kwenye kampasi zote tatu za Chuo Kikuu cha SUA 
Pia kupitia  mradi huo SUA imejenga jengo la maabara mtambuka ambalo linauwezo wa kuchukua wanafunzi 3,200 kwa wakati mmoja kupata mafunzo.
#BiMkubwaKazini