DKT SAMIA APONGEZWA,KUFUFUA CHUO KILICHOSIMAMA KWA MIAKA 20

 

DKT SAMIA APONGEZWA,KUFUFUA CHUO KILICHOSIMAMA KWA MIAKA 20

DKT SAMIA APONGEZWA,KUFUFUA CHUO KILICHOSIMAMA KWA MIAKA 20

TABORA 
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imempongeza Rais Dkt  Samia Suluhu Hassan kwa kufufua Chuo cha Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu Wenye Ulemavu Rwenzari ambacho kilikuwa hakifanyi kazi takribani miaka 20.
Serikali ya awamu ya sita imetoa Shilingi milioni 689 kwa ajili ya kukarabati chuo hicho kwa kununua samani, upanuzi wa kuta na vifaa kwa ajili ya wanafunzi kujifunzia na kina uwezo wa kuchukua wanafunzi 129 katika kozi za uselemara, ubunifu ushonaji, kilimo bustani, uchomereaji na umeme wa majumbani.
Aidha mafunzo wanayopata wanafunzi chuoni hapo yatawasaidia kujiajiri na kuanzisha mafunzo kwa watu wengine ili kuinua uchumi wao na taifa kwa ujumla.
Akitoa neno la shukrani mwanafunzi wa chuo hicho Amosi Yokram amemshuru Rais kwa kuendelea kuwajali watu wenye ulemavu na kuboresha miundombinu kwa ajili ya kupata elimu.
Muhimu:- Dhamira ya  Rais Dkt  Samia ni kuhakikisha makundi ya watu wenye ulemavu wanapata fursa sawa za kushiriki katika kujenga taifa lao na kuishi katika mazingira salama.