TSH BIL 42 KUWANYANYUA WANANCHI WA IFAKARA

 

TSH BIL 42 KUWANYANYUA WANANCHI WA IFAKARA

TSH BIL 42 KUWANYANYUA WANANCHI WA IFAKARA

MOROGORO
Serikali ya awamu ya sita imetoa kiasi  cha shilingi bilioni 42 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji  mseleleko  kutoka katika chanzo cha mto kiburubutu  uliopo katika Halmashauri ya Mji Ifakara ambao umeanza kutekelezwa mwaka 2023  huku ukitarajiwa kukamilika mwezi oktoba 2025.
Mradi huo ukikamilika utazalisha jumla ya lita za uzajo milioni 20 kila siku na kuondoa tatizo la maji ambapo kwa sasa Mji wa Ifakara una wakazi wapatao laki moja na elfu arobaini kutoka katika kata tisa za Halmashauri ya Mji Ifakara mkoani Morogoro huku upatikanaji  wa huduma ya maji ukiwa ni ujazo wa lita milioni 1.3 wakati uhitaji ni jumla ya ujazo wa lita milioni 10 kwa kila siku.