TAZARA NA TPSF KULETA TRENI ZA MIZIGO
DAR ES SALAAM
Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (Tazara) limesaini mkataba wenye thamani ya shilingi bilioni 20 na sekta binafsi ambapo mkataba huo utawawezesha sekta binafsi kuleta treni ambazo zitatoa mzigo bandarini kwenda kwenye nchi zinazozunguka ukanda wa SADC ikiwemo Zambia na Congo.
Mkataba huo umesainiwa Machi 20, 2024 Makao Makuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam kati ya Tazara na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) ikiwakilishwa na Mwenyekiti wake Bi. Angelina Ngalula.
Akizungumza Ching’andu amesema makubaliano hayo yanalenga kupanua ukuaji wa uchumi na fursa za biashara ndani ya ukanda wa Dar es Salaam sambamba na kuimarisha biashara ya ndani ya Kanda ya SADC.
Nae, Mwenyekiti wa TPSF, Angelina Ngalula ametoa shukrani kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya biashara ambayo yanahimiza uwekezaji na ukuaji wa biashara, na kusababisha fursa za ajira na michango chanya katika Pato la Taifa (GDP).
Kwa mkataba huo,
