TSH BIL 4.3 ZA MRADI WA MAJI NZUNGUNI NI 99%
DODOMA
Serikali kupitia DUWASA inaendelea kutekeleza mradi wa maji safi Nzuguni kwa shilingi bilioni 4.3 fedha za mapato ya ndani,lengo likiwa ni kuboresha huduma ya usambazaji maji katika kata na jiji la Dodoma kwa ujumla, kwa kuongeza uzalishaji wa maji kutoka lita 68,600,000 hadi 76,000,000 kwasiku, sawa na ongezeko la 11.7%
Hadi sasa mradi umefikia 99% na unatekelezwa na wazabuni saba ambao ni TANESCO, Tanelec Limited Arusha, Master Drillingand Exploration Ltd, Help DeskLtd, Davis Shitriff Ltd, JudexContractors na Tanzania SteelPipes.
Mradi huo umehusisha uchimbaji na uendelezaji wa visima vinne,ununuzi wa transfoma sita, ujenzi wa mtandao wa kusafirisha na kusambaza maji wenye takriban kilomita saba, ujenzi wa matangi mawili yenye jumla ya ujazo wa lita 3,500,000 na ujezi wa vibanda vya kuendeshea pampu
