TANZANIA YATEKELEZA 80% YA TSMP
DAR ES SALAAM
Tanzania imetekeleza asilimia 80 ya shughuli zilizopangwa kutekelezwa katika mwaka wa pili wa Mpango Mkuu wa Pili wa Taifa wa Takwimu (TSMP II) ambao awamu ya kwanza ulianza Agosti 2022 na awamu ya pili ya utekelezaji wake ulianza Agosti mwaka 2023
TSMP II, unatekelezwa kuanzia 2022 hadi 2027 chini ya serikali kupitia Benki ya Dunia (WB).
TSMP inakusudia kuoanisha takwimu katika taasisi za serikali, kuimarisha takwimu za utawala na miundo msingi katika kukusanya takwimu, aidha kazi zilizokamilika katika awamu ya pili ni pamoja na utafiti wa nguvu kazi.
Mwaka 2022 Tanzania ilivunja rekodi kwa kutoa ripoti ya sensa ndani ya siku 45 baada ya kukusanya takwimu, hatua ikiwa ni utekelezaji wa mpango huo
