TSH BIL 132.016 KUWAVUSHA MOROGORO
MOROGORO
Serikali ya awamu ya sita kupitia TANROADS imesaini mkataba wa Ujenzi wa barabara ya Bigwa – Kisaki; sehemu ya Bigwa –Mvuha, km 78; ambao una thamani ya shilingi bilioni 132.016.
Mkataba huo umesainiwa Februari 2024, na Mkandarasi M/s China railways 15 Bureau Group Corporation ya China atatekeleza mradi huo kwa muda wa miezi 27 kuanzia Februari 2024.
