TSH BIL 11.3 KUJENGA MAJENGO HOSPITALI YA RUFAA SHINYANGA.

 

TSH BIL 11.3 KUJENGA MAJENGO HOSPITALI YA RUFAA SHINYANGA.

TSH BIL 11.3 KUJENGA MAJENGO HOSPITALI YA RUFAA SHINYANGA.

SHINYANGA
Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha hali ya utoaji wa huduma za Afya Mkoani Shinyanga kwa kupanga kujenga majengo ya kisasa yenye thamani ya Shillingi Bilioni 11.3 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.
Chanzo:- Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe wakati wa makabidhiano ya eneo la ujenzi na Mshauri elekezi wa masuala ya ujenzi Katika eneo la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Shinyanga, zoezi lililofanyika Shinyanga Februari 23, 2024.
Ujenzi huo unatarajiwa kuongeza majengo mapya matano ambayo ni jengo la ghorofa tatu la huduma za afya ya mama na mtoto, maabara ya kisasa, jengo la kufulia nguo, jengo la dawa na jengo la kuhifadhia maiti na hivyo kuo
ngeza wigo wa utoaji wa huduma kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Pia ujenzi wa jengo la nje (OPD) unaendelea,na jengo hilo litatoa huduma zote za wagonjwa wa nje ikiwemo upasuaji mdogo.
Aidha jengo hilo linajengwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na linagharimu shilingi milioni 486 na linatarajia kukamilika ifikapo Machi 31, 2024.
FAIDA:-Ujenzi wa jengo hilo utapunguza msongamano wa wagonjwa katika kituo cha Afya Kambarage na pia kuboresha huduma za dharura.