DKT SAMIA APONGEZWA , UCHUMI SHIRIKISHI
DODOMA
Falsafa ya uchumi shirikishi ambayo Mhe Rais Dkt Samia amekuwa anaifanya katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi, kiuongozi na kijamii kwa wanawake zimekuwa chachu ya kugusa na kuibua makundi mbalimbali ya wanawake kuonesha hisia zao juu ya hatua hizo zinazochukuliwa na mkuu wa nchi.
Miongoni mwa wanaoguswa na jitihada hizo ni wanawake wa Mkoa wa Dodoma ambao wamempongeza Mhe Rais Dkt Samia kutokana na kazi kubwa anayoifanya katika kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika uchumi jumuishi.
Wakizungumza Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya jukwaa la uwezeshaji wanawake Mkoani Dodoma ambapo wamesema uanzishwaji wa majukwaa ya aina hiyo yamekuwa chachu kubwa katika kuwawezesha wanawake kiuchumi pamoja na kuwaratibu kwa fursa mbalimbali za kuboresha uchumi wao binafsi.
“Mkuu wa Nchi anatudai kura zake katika Uchaguzi Mkuu ujao, kwa hiyo, tunatakiwa kumpigia kura nyingi sana kwa sababu ya yale ambayo amekuwa akitufanyia siku zote,’’amesema Bi Tawfiq anayewakilisha wanawake Mkoa wa Dodoma.
Bibi Tawfiq pia amebainisha kuwa serikali ya awamu ya sita imeweka miundombinu inayofaa na rafiki katika shule, hospitali na huduma nyingine za kijamii, jambo ambalo linawafanya wanawake na watoto wao kuishi maisha ya starehe.
Aidha serikali chini ya Rais Dkt Samia imekuwa ikisisitiza mara kwa mara kuwa imejipanga kutekeleza ahadi za kikanda na kimataifa ili kuhakikisha kunafikiwa kwa usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake.
KUMBUKA:-Ajenda ya uwezeshaji wanawake, ni miongoni mwa Malengo 17 ya Maendeleo ya Milenia ya 2000, ambapo lengo namba 3 linalenga kuwawezesha wanawake na kukuza usawa wa kijinsia.
