TSH BIL 10.7 KUIMARISHA HAKI KWA WANAWAKE
DAR ES SALAAM
Kituo cha Huduma za Kisheria (LSF) na Enabel, wakala wa maendeleo wa Ubelgiji, wametia saini makubaliano ya ruzuku ya shilingi bilioni 10.7 ili kutekeleza Mradi wa Kuboresha Upatikanaji wa Haki kwa Wanawake kupitia Msaada wa Kisheria (IMPAWLA).
Kupitia mradi wa LSF utahakikisha huduma za msaada wa kisheria za hali ya juu zinapatikana kwa watu wote kupitia mifumo ya utoaji haki rasmi na isiyo rasmi, kuwezesha jamii kuelewa, kuunda na kutumia sheria.
Akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini Mwakilishi Mkazi wa Kampuni ya Enabel nchini Tanzania, Koenraad Goekint amesema shirika hilo limefurahi kushirikiana na LSF ili kuhakikisha upatikanaji wa haki nchini
“Ushirikiano huu unasisitiza dhamira yetu ya kukuza maendeleo endelevu na kukuza jamii ambapo kila mtu anaweza kupata haki zake na kushiriki kikamilifu katika mfumo wa sheria.
Kwa kutumia utaalamu na rasilimali zetu za pamoja, tunalenga kupiga hatua za maana katika kujenga jamii yenye usawa na haki kwa Watanzania wote,” Goekint amesema.
