KAHAWA YA TANZANIA YAWA KIVUTIO JAPAN

 

KAHAWA YA TANZANIA YAWA KIVUTIO JAPAN

KAHAWA YA TANZANIA YAWA KIVUTIO JAPAN

JAPAN
Kahawa ya Tanzania imeendelea kulishika soko la kimataifa baada ya  Kampuni ya ITO EN LTD, ambayo ni kampuni tanzu ya Tully’s Co. Ltd. inayomiliki migahawa maarufu ya Tully’s Coffee, kuzindua aina tatu mpya za kahawa ya Tanzania nchini Japan katika hafla iliyofanyika jijini Tokyo Machi 14, 2024.
Kahawa zinazopendwa zaidi Nchini Japan ni kutoka mkoa wa Arusha, Tarime mkoani Mara na mashamba ya GDM yaliyoko Mbozi mkoani Mbeya.
Tukio hilo la uzinduzi limefanyika Machin 14  katika Ubalozi wa Tanzania jijini Tokyo likiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Japan, Baraka Luvanda na kumshirikisha Meneja Mkuu wa Kampuni ya ITO EN Osamu Aizawa,  aliyeambatana na wawakilishi wa kampuni hiyo na Kampuni yaTully’s Coffee.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Balozi Baraka Luvanda amezihakikishia kampuni za Japan, uwepo wa mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji wanapoamua kuwekeza katika kilimo au sekta nyinginezo hapa nchini.
Balozi Luvanda amelitaja zao la kahawa kuwa ni miongoni mwa mazao ya kimkakati yanayoongoza kwa kulipatia Taifa pato na kuingiza fedha za kigeni.
Aidha, Balozi Luvanda ameelezea juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na  Rais Samia Suluhu Hassan, kuwa imefanya mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo.