TANZANIA YAPELEKA WANARIADHA 75 (ALL AFRICA GAMES 2024 )
DAR ES SALAAM
Tanzania imepeleka rasmi wanariadha 75 watakaoshiriki katika fani mbalimbali za kimichezo katika mashindano yajayo ya All Africa Games 2024 yatakayofanyika Accra, Ghana, kuanzia Machi 8 hadi Machi 23 huku maelfu ya wanariadha kutoka sehemu zote za bara wakipigania medali.
Chanzo:- Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo
Wanariadha watakaoondoka watashiriki mashindano ya Baiskeli, Riadha, Kuogelea, Ngumi, Kriketi, Judo na Timu ya Soka ya Wanawake chini ya umri wa miaka 20 ‘Tanzanite.
KILA LA KHERI WATANZANIA, MKASHINDANE ILI KUSHINDA
