RIPOTI - TANZANIA NI SALAMA KWA WASAFIRI AFRIKA
KENYA
Tovuti ya 𝑺𝒂𝒇𝒂𝒓𝒊 𝑩𝒐𝒐𝒌𝒊𝒏𝒈𝒔 inayojihusisha na masuala ya kupanga safari za Kiafrika yenye makao makuu yake katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda imetoa orodha ya nchi 10 bora salama zaidi barani Afrika kwa mwaka 2024 kwa kuzitembelea.
Katika orodha ya nchi hizo 10, 𝗧𝗮𝗻𝘇𝗮𝗻𝗶𝗮 imeshika nafasi ya kwanza kwa bara zima la Afrika ambapo sababu zilizoanishwa na safari Bookings ni pamoja na wingi na aina mbalimbali za wanyamapori wake, pamoja na weledi wa waongoza safari kwenye maeneo ya vivutio/mbugani.
“Tanzania kwa ujumla ni salama kwa wasafiri , ziara nyingi hazina uhalifu. Watu wengi watakuwa wakisafiri nje ya miji, jambo ambalo linapunguza hatari ya uhalifu. Safaris kwa kawaida ni salama sana na waelekezi waliohitimu wanajua jinsi ya kushughulikia wanyamapori kukutana” imesema ripoti hiyo.
Maeneo mengine yaliyotajwa ni Kenya , Botswana , Uganda ,Namibia ,Zambia , Rwanda ,Mauritius,Seychelles na Lesotho.
