TANZANIA ,UINGEREZA KUTAFUTA NJIA MPYA ZA UFADHILI
UINGEREZA
TANZANIA na Uingereza zinatafuta mbinu mpya kupitia Mfuko wa Fedha wa Mauzo ya Nje wa Uingereza (UKEF) ili kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili ndani ya mfumo wa ushirikiano wa pamoja.
Chanzo:- Mjumbe wa Biashara wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Lord Walney kupitia kikao cha mtandao(zoom) kilichowaleta pamoja wadau kutoka sekta ya umma na binafsi ya Tanzania na wawakilishi kutoka UKEF.
Mkutano huo wa mtandaoni ulijumuisha wawakilishi kutoka sekta za fedha na benki za Tanzania, Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na sekta ya madini.
Kupitia mkutano huo Bwana Lord Walney, amesema lengo la mkutano huo wa mtandaoni lilikuwa kutafuta njia ambazo UKEF inaweza kuimarisha uhusiano kati ya Uingereza na Tanzania ndani ya mfumo wa ushirikiano wa pande zote.
Mkuu mwenza wa Global Origination Africa na America kupitia UKEF, Bi Emma Thomas amesema Uingereza imetenga kiasi cha paundi bilioni 2.5 (takribani shilingi trilioni 8 za Kitanzania.
kwa sasa, UKEF inasaidia miradi ya Zanzibar yenye thamani ya paundi milioni 373 (zaidi ya shilingi trilioni 1.2 fedha ya Tanzania)
#PumzikaKwaAmaniMzeeMwinyi