JAJI MKUU AIPONGEZA SERIKALI MKOPO WA TSH BIL 386+ (WB) KUBORESHA MAHAKAMA

 

JAJI MKUU AIPONGEZA SERIKALI MKOPO WA TSH BIL 386+ (WB) KUBORESHA MAHAKAMA

JAJI MKUU AIPONGEZA SERIKALI MKOPO WA TSH BIL 386+ (WB) KUBORESHA MAHAKAMA

DODOMA
Serikali imepongezwa kwa kuchukua mkopo  kutoka benki Dunia (WB) wa jumla shilingi 386,840,000,000 kwa ajili ya kuboresha miundombinu na huduma za mahakama nchini.
Pongezi hizo zimetolewa na Jaji mkuu wa mahakama ya Tanzania Profesa Ibrahim Juma mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria Nchini yaliyofanyika tarehe 1,Februari 2024 Katika viwanja vya Chinagali Jijini Dodoma.
Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Profesa Ibrahim amesema mikopo iliyochukuliwa na serikali kwa awamu mbii tofuati ( dola milioni 61 awamu ya kwanza sawa na shilingi bilioni 155,245,000,000 na dola milioni 91 sawa na shilingi bilioni 231,595,000,000) imeonesha dhamira ya wazi ya serikali kuboresha na kuharakisha upatikanaji wa haki nchini.
Aidha Profesa Ibrahimu amesema “bila uwekezaji mkubwa wa serikali mahakama haiwezi kufanya lolote katika kufanikisha haki, tusingeweza kufika hapa bila sera nzuri ambazo zimetuwezesha kufanikisha matumizi ya TEHAMA”
KUMBUKA:- Maadhimisho ya wiki ya sheria hufanyika kila mwaka kuashiria kuanza kwa mwaka mpya wa kazi wa mahakama na mwaka huu yalianza tarehe 24 hadi 30 Januari.