SERIKALI INASHIRIKIANA NA MAHAKAMA KUTATUA CHANGAMOTO –DKT SAMIA

 

serikali inashirikiana na mahakama kutatua changamoto

SERIKALI INASHIRIKIANA NA MAHAKAMA KUTATUA CHANGAMOTO –DKT SAMIA

DODOMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inaendelea na mkakati wa kutekeleza mapendekezo mengine yaliyotolewa na ripoti ya tume ya haki jinai ya kisera na kisheria na kwa kufanya hivyo pia ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi 2020-2025 ibara ya 120 ambayo inaitaka serikali pamoja na mambo mengine kuchukua hatua zaidi ya kupunguza mlundikano wa kesi mahakamani,kuimarisha vyombo vya sheria kwa kuongeza wigo wa kutoa huduma za utoaji wa haki nchini na kujenga mifumo ya TEHAMA na kuendeleza kuhimiza matumizi yake katika utoaji wa haki.
Rais Samia ameyasema hayo leo Februari mosi, 2024 kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini yaliyofanyika katika viwanja vya chingali Jijini Dodoma.
Dkt Samia amesema pamoja na uwekezaji mkubwa kwenye TEHAMA, serikali pia imeendelea kuimarisha utendaji wa mahakama kwa ujenzi wa majengo ya kisasa ya mahakama(vituo jumuishi vya kutolea haki) na kuongeza idadi ya watenda kazi.
KUMBUKA:- Idadi ya majaji wa mahakama ya rufani imeongezeka kutoka majaji 16 mwaka 2021 hadi 35 (pamoja na jaji mkuu) 2023, Majaji wa mahakama kuu imeongezeka kutoka 63 mwaka 2021 hadi 105 mwaka 2023.