RIPOTI-TANZANIA YATAJWA NCHI YENYE DEMOKRASIA DUNIANI
UINGEREZA
Tanzania imetajwa kuwa ni miongoni mwa nchi zenye demokrasia safi ulimwenguni huku ikishika nafasi ya kwanza kwa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC).Ripoti ya hali ya demokrasia duniani iliyoandaliwa na Economist Intelligence Unit (EIU) kupitia ripoti yake ya “Democracy Index 2023” imeangazia hali ya demokrasia katika nchi 165 ambapo Vigezo vilivyotumika kupima hali ya demokrasia katika mataifa hayo vimezingatia mambo kadhaa, ikiwemo mchakato wa uchaguzi na mfumo wa vyama vingi, utendaji kazi wa Serikali, ushiriki wa kisiasa, utamaduni wa kisiasa na uhuru wa wananchi.
Kwa kuzingatia vigezo hivyo, kila nchi inawekwa kwenye kundi lake kati ya makundi manne ya utawala ambayo ni demokrasia kamili, demokrasia yenye upungufu, utawala mseto na utawala wa kiimla.
Kwa upande wa alama, Tanzania inaongoza katika nchi za Afrika Mashariki ikishika nafasi ya 12 kikanda na kidunia nafasi ya 86, ikifuatiwa na Kenya nafasi ya 14 kikanda na 92 kidunia wakati Uganda inashika nafasi ya 16 kikanda na 99 kidunia
MAONI YA WADAU KUHUSU NAFASI HII YA TANZANIA
Mwanazuoni wa sayansi ya siasa na sheria kutoka Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (LST), Profesa Ambrose Kessy anasema nafasi ya Tanzania kwenye ripoti hiyo si jambo la kushangaza kwa sasa kutokana na Rais aliyepo madarakani (Samia Suluhu Hassan).
“Serikali ya sasa imebadilika, imetoa uhuru mkubwa kwa watu kujieleza bila kuvunja sheria na nafikiri imejitathimini na kuona kila mtu anayo nafasi ya kufanya mapinduzi katika taifa iwapo atapewa nafasi,” anasema Kessy.
Kessy amaeongeza “Rais Samia amejitahidi kufanya mengi na yote hayo yanaonekana ni katika kuionesha dunia tunakua kutoka chini ambako watu walikuwa wanalalamika kutokuwa na uhuru hasa vyama vya upinzani,”
Nae, Dkt Paul Loisuilie Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) anasema 4R imechangia kwa kiwango kikubwa katika kipindi hiki na imesaidia kuleta mapinduzi ya siasa za Tanzania,
“Ndani ya kipindi hiki ustahimilivu umeshamiri kwa kiwango kikubwa kwa viongozi wa kiserikali,kitendo cha kuacha uhuru wa watu kupumua kusema ya kwao imeleta ufanisi mkubwa.Pia hata Rais mwenyewe anaonesha utashi mkubwa wa kisiasa, anastahimili vya kutosha kwa kuamini nchi inapaswa kujengwa na wote kwa kuruhusu kila mmoja kutoa mawazo yake,” anasema.
Amesisitiza kwamba ndani ya kipindi cha miaka miwili nyuma Serikali imekuwa ikifanya maridhiano na vyama vya siasa na utulivu unazidi kuongezeka na ni eneo ambalo hata Kenya wamezidiwa.
#PumzikaKwaAmaniMzeeMwinyi