BARABARA YA BUNAZI YAKAMILIKA

 

BARABARA YA BUNAZI YAKAMILIKA

BARABARA YA BUNAZI YAKAMILIKA

KAGERA
Serikali kupitia wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (Tarura), Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera imekamilisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami eneo la Bunazi, Kata Kasambya.
Kujengwa kwa barabara hiyo kwa kiwango cha lami imewezesha wananchi kupita kiurahisi na kuleta faida kama kukua kwa shughuli za kiuchumi na kuondoa matengenezo ya mara kwa mara
Hapo awali  Wilaya ya Missenyi bajeti ya barabara ilikuwa ni Sh milioni 700 tu, lakini hivi sasa wilaya inapokea Sh bilioni 2.4 kwa mwaka.