MHE RAIS SAMIA KUONGOZA WAOMBOLEZAJI HAYATI MWINYI AKIZIKWA MACHI 2

 

MHE RAIS SAMIA KUONGOZA WAOMBOLEZAJI HAYATI MWINYI AKIZIKWA MACHI 2

MHE RAIS SAMIA KUONGOZA WAOMBOLEZAJI HAYATI MWINYI AKIZIKWA MACHI 2

DAR ES SALAAM 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan  anatarajiwa kuongoza salamu za pole kutoka kwa makundi mbali mbali kufuatia kifo cha Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kilichotokea Februari 29,2024.
Mwili wa Rais wa Awamu ya Pili, Hayati Ali Hassan Mwinyi unatarajiwa kupumzishwa kesho Machi 2, 2024 saa 10: 30 jioni katika kijiji cha Mangapwani visiwani Zanzibar.
Mwili wa Hayati Rais Mwinyi umeswaliwa katika Msikiti Mkuu wa Bakwata Kinondoni jijini Dar es Salaam, na saa nane  mchana mwili wa Hayati Mwinyi utaelekea uwanja wa Uhuru, dua na salamu mbali mbali za rambirambi zitatolewa na viongozi na wananchi watapata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho.
Kuanzia saa 11 jioni mwili wa Hayati Mzee Mwinyi utaondoka uwanja wa Uhuru na kuelekea uwanja wa ndege tayari kwa safari ya Zanzibar ambapo Wananchi wa Zanzibar wataupokea mwili wa Mzee Mwinyi uwanja wa ndege wa Abeid Karume kuanzia saa 11 jioni (leo) ambapo (kesho) tarehe 2 Machi 
 saa nne mwili utaondoka nyumbani kuelekea uwanja wa Amani kwa maombolezo ya kitaifa na kuanzia saa 6:30 wananchi na viongozi mbali mbali watapata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho kisha  atapumzishwa kijijjini Manga Pwani saa 10 jioni.