TANZANIA, PAKISTAN KUSHIRIKIANA KIBIASHARA
DAR ES SALAAM
Tanzania na Pakistan zimeahidi kuendelea kushirikiana kuimarisha zaidi sekta za biashara na uwekezaji kwa maslahi ya pande zote mbili, huku sekta za elimu, afya, ulinzi, kilimo, nishati uchumi wa buluu na usafirishaji zikipigiwa chapuo.
Ahadi hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Asia na Australia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Salvastory Mbilinyi alipokutana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan, Shehryar Akbar Khan katika majadiliano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na Pakistan.
Chimbuko la majadaliano hayo ni kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Pakistan pia Serikali ya Tanzanzia imejikita zaidi katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini hivyo wafanyabiashara kutoka Pakistan wamepata ari ya kuwekeza Tanzania.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan, Shehryar Akbar Khan amesema Pakistan na Tanzania zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu na zimekuwa zikishirikiana katika sekta mbalimbali wakati wote.
“Nchi zetu zimekuwa zikishirikiana katika sekta mbalimbali, ila kwa sasa tunaona ni vyema tukaimarisha zaidi sekta ya biashara na uwekezaji kwani kila nchi inahitaji biashara na uwekezaji,” amesema Khan.
#NguvuyaDiplomasia
