2021/2022 MTWARA WALIPEWA TSH BIL 264+
MTWARA
Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan katika mwaka wa fedha 2021/22 iliidhinisha kiasi cha shilingi 264,338,522,589.00 (Bilioni 264.34) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na Matumizi ya Kawaida kwa Mkoa wa Mtwara.
Kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni 7.64 ni kwa ajili ya Sekretarieti ya Mkoa ambapo Shilingi Bilioni 2.73 ni kwa ajili ya kulipa mishahara, na Shilingi Bilioni 2.49 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo na Shilingi Bilioni 2.42 kwa ajili ya miradi ya maendeleo, pamoja na Shilingi Bilioni 256.69 kwa ajili ya Halmashauri ambapo Shilingi Bilioni 117.73 kwa ajili ya mishahara, Shilingi Bilioni 25.47 kwa ajili ya matumizi mengineyo na Shilingi Bilioni 113.49 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
#BiMkubwaKazini
