TANZANIA NCHI YA KWANZA BARANI AFRIKA KUTUMIA TTS
DODOMA
Tanzania imekuwa nchi ya kwanza Barani Afrika kutumia Mfumo wa Unukuzi na Tafsiri (TTS) mahakamani, hii ni kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel
Prof. Ole Gabriel ameyasema hayo tarehe 17 Machi, 2024 wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ilipotembelea Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) Dodoma kwa lengo la kukagua Mfumo huo.
“Kwa kifupi napenda niseme tu kwamba Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria imeguswa na kuridhishwa na matumizi ya teknolojia hii na kwa Afrika, Tanzania ndio itakuwa Nchi ya kwanza kutumia Mfumo huu,” amesema Mtendaji Mkuu.
Amesema, Mahakama inazidi kuongeza kasi kwenda kidijiti na hakuna namna juhudi hizo zitarudi nyuma (no reverse gear) na kwamba kwa sasa Mhimili huo una mifumo ya Kitehama ipatayo 11.
Kadhalika, Prof. Ole Gabriel amesema kwamba, Mfumo wa TTS unasimamiwa na Idara ya TEHAMA kwa kushirikiana kwa karibu na Mamlaka ya Serikali Mtandao ‘e-GA’
