MAJI YA ZIWA VICTORIA KUHUDUMIA DODOMA
DODOMA
Katika kuhakikisha Dodoma inakuwa na maji ya uhakika katika mipango ya muda mrefu, serikali imepanga kuanza kutekeleza mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria hadi Dodoma.
Mradi huo utahusisha ujenzi wa mtambo wa kutibu maji,matangi, vituo vya kusukuma maji na mabomba ya kusafirisha maji kutoka Mwanza hadi Dodoma.
Serikali kupitia Wizara ya Maji imeshatangaza zabuni ya Mhandisi Mshauri wa kufanya upembuzi yakinifu,usanifu, zabuni za mkandarasi wa ujenzi na kusimamia utekelezaji wa mradi huu, ambapo Wizara imewasilisha mkataba wa kazi hii kwa Mwanasheria Mkuu kwa uchunguzi.
#BiMkubwaKazini
