TANZANIA NA IRAQ KUIMARISHA UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA

 

TANZANIA NA IRAQ KUIMARISHA  UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA

TANZANIA NA IRAQ KUIMARISHA  UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA

UTURUKI
Tanzania na Iraq zinatafuta namna bora zaidi ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia hasa kwa manufaa ya mabunge ya nchi hizo mbili (Tanzania & Iraq)
Hatua hii imekuja kutokana na mazungumzo kati ya Spika wa Bunge la Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge (IPU), MhTulia Ackson na Naibu Waziri Mkuu wa Iraq na Waziri wa Mambo ya Nje, Dkt Fuad Hussein
kando ya Jukwaa la Diplomasia la Mjini Antalya nchini Uturuki.
Zaidi ya hayo, wawili hao (kwa niaba ya nchi zao) walizungumzia jinsi ya kuweka amani na usalama katika Mashariki ya Kati kupitia njia za kidiplomasia, kwa kutumia Iraq kama mfano wa kuigwa kwa sababu ya historia yake na namna, ambayo iliweza kupata uhuru na kuanzisha msingi imara wa kidemokrasia.