STAMICO KUANZA MRADI WA UZALISHAJI MADINI UJENZI
DODOM
Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa ( STAMICO) linatarajia kuanza mradi wa uzalishaji wa madini ujenzi aina ya kokoto katika eneo la Chigongwe mkoani Dodoma ambapo unatarajia kuzalisha tani 150-200 kwa saa na tani 2000 kwa siku.
Hadi sasa utafiti umeonesha kuwepo kwa kiasi cha tani 13.1 cha akiba ya malighafi itakayovunwa kwa kipindi cha miaka nane kwa awamu ya kwanza katika leseni mbili kati ya kumi zilizopo na uzalishaji huu mpya utakapo anza 20% imelengwa katika ujenzi wa makazi na 80% zitaenda katika miradi ya maendeleo kama vile ujenzi wa barabara, reli na viwanja vya ndege na michezo .
Mradi huo wa kimkakati utatatua changamoto ya kukosekana kwa madini ujenzi katika miradi ya maendeleo ndani na nje ya mji wa Dodoma.
