DKT SAMIA AKUTANA NA MA-RAIS MUSEVENI & RUTO
ZANZIBAR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais William Ruto wa Kenya katika Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar tarehe 14 Machi, 2024.
Kwenye mazungumzo yao wamegusia masuala ya mtangamano wa Afrika Mashariki hususan umuhimu wa kuharakisha zoezi la kukusanya maoni ya Wananchi Juu ya muundo na maeneo ya kuangaliwa katika Rasimu ya Katiba ya Fungamano la kisiasa la Afrika Mashariki (EAC Political Confederation).
Zoezi hilo limeshafanyika katika nchi za Burundi, Uganda na Kenya na linatekelezwa na Timu ya Wataalamu inayoundwa na Wajumbe watatu kutoka kila nchi Mwanachama.
