RUZUKU YA MBOLEA YAFIKIA TSH BIL 200
DAR ES SALAAM.
Serikali ya awamu ya sita imefanikisha kuongeza matumizi ya mbolea kutoka tani 363,600 mwaka 2021/22 hadi tani 580,600 mwaka 2022/23 hii ni kutokana na utolewaji wa ruzuku ya mbolea kwa wastani wa billioni 200 kuanzia mwaka 2022/23
Makadirio ya serikali kupitia wizara ya kilimo ni kufikisha jumla ya shilingi trilioni 1 ifikapo mwaka 2025/26 ambapo itaongeza matumizi ya mbolea hadi kufikia tani 1,000,000
Kuelekea kufanikisha kwa mpango huu wizara ya kilimo chini ya serikali imefufua Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) na kuipa mtaji wa jumla ya Shilingi bilioni 116 kwa ajili ya kufanya biashara ya mbolea nchini na sasa imekuwa moja ya makampuni 6 bora kati ya makampuni 30 ya usambazaji wa mbolea hapa nchini.
Aidha kampuni hii inaongoza katika eneo la usambazaji wa mbolea kwa kuwafikia wakulima wa mikoa 26 na Halmashauri 104.
