RIPOTI- DKT SAMIA MICHEZONI KWA MIAKA MITATU
Wakati ikibaki siku moja kabla ya Mhe Rais Dkt Samia kutimiza miaka mitatu ya uongozi wake (Machi 19,2021 –Machi 19,2024) BimkubwaTanzania inakuonesha ni kwa namna gani serikali ya awamu ya sita imekuwa ikigusa moja kwa moja sekta ya michezo
Ndani ya kipindi ch miaka mitatu, Mhe Rais Dkt Samia amejitanabaisha kuwa mdau mkubwa wa sekta ya michezo kutokana na ushiriki wake katika shughuli mbalimbali za sekta hiyo pamoja na mipango mbalimbali ambayo uongozi wake umeiweka ili kuhakikisha michezo inapiga hatua Nchini.
Ushiriki Dkt Samia katika michezo umeonekana kujenga imani ya wengi kuwa huenda sekta ya michezo ikapata mafanikio makubwa chini ya utawala wake,
Ipo mifano na uthibitisho wa wazi unaoonesha jinsi Rais Samia anavyotamani kuona michezo sio tu inakuwepo kwa ajili ya kujifurahisha bali kugeuka fursa ya ajira na kukuza uchumi wa nchi.
UDHAMINI SOKA LA WANAWAKE CECAFA
Agosti 21, 2021, Rais Samia alikubali ombi la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) la kuwa mdhamini wa mashindano ya wanawake ya Cecafa.
SERENGETI GIRLS NCHINI INDIA KOMBE LA DUNIA LA FIFA 2022 :- Serikali ya awamu ya sita ilichukua jukumu kubwa katika kuunga mkono timu ya Serengeti girls (U-17), kuwezesha kambi ya makazi katika nchi ya England( Nje ya Nchi ambayo mashindano yalikuwa yakifanyika) ambapo walishiriki katika mfululizo wa mechi za maandalizi kuelekea michuano kufanikisha kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia la FIFA 2022 nchini India.
TEMBO WARRIORS KATIKA KOMBE LA DUNIA LA AMPUTEE 2022, UTURUKI :- Kujitolea kwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika michezo kuliwezesha timu ya Taifa ya Soka kwa Walemavu, (Tembo Warriors) kuweka kambi ya makazi ndani na nje ya nchi, kuelekea ushiriki wa timu hiyo kuwa miongoni mwa timu 24 zilizoshiriki katika hatua ya 16/17 ya Kombe la Dunia lililofanyika Istanbul, Uturuki, kuanzia Septemba 30 hadi Oktoba 9, 2022.
KUNUNUA KILA GOLI MECHI ZA KIMATAIFA :- Utawala wa Rais Samia mwaka 2022, ulianzisha utaratibu wa kuzipa hamasa klabu za Tanzania zilizokuwa zinashiriki mashindano ya klabu Afrika kwa kutoa kiasi cha Sh 5 milioni kwa kila bao ambalo zilikuwa zinafunga kuanzia hatua ya makundi na kuendelea.
UJENZI,UKARABATI WA VIWANJA:- Wakati wa utawala wa Rais Samia unaingia madarakani uliahidi utatenga bajeti ya fedha kwa ajili ya kusaidia maboresho ya viwanja vya soka katika maeno mbalimbali nchini (Rejea marekebisho/maboresho ya uwanja wa Benjamini Mkapa ambao kiasi cha shilingi bilioni 31 zinakadiriwa kuuboresha uwanja huo)
KUTOA NDEGE KWA TIMU YA YANGA :- Mei 2023 Mhe Rais Dkt Samia alitoa ndege binafsi (Boeing 787-8 Dreamliner ) kwa ajili ya kupeleka timu, viongozi na mashabiki wa timu ya Yanga katika hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika waliyocheza na Algers USM Alger ya Algeria tarehe 3 Juni, 2023
MHE.RAIS DKT SAMIA KUWA MGENI RASMI,SIMBA DAY :-Agosti 6 Mwaka 2023 Mhe Rais Dkt Samia Suluhu alikubali kuwa mgeni rasmi kwenye tamasha la Simba Dat lililofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa
KUANDAA AFCON 2027 :- Uongozi wa Rais Samia ulianzisha wazo la kuomba kuandaa fainali za mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka 2027, Kutokana na hilo, ilishauriwa kwamba ni vyema Tanzania ingeomba kuandaa kwa pamoja mashindano hayo na nchi za Kenya na Uganda ambazo ipo nazo pamoja katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, lakini pia ni wanachama wa baraza la vyama vya mpira wa miguu Afrika Mashariki na Kati(Cecafa).
TWIGA STARS KUFUZU KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA KWA WANAWAKE CAF 2024 :- Mafanikio mengine makubwa katika maendeleo ya michezo yamefikiwa na timu ya taifa ya wanawake ya wakubwa, Twiga Stars, ilipofuzu kwa mara ya kwanza kushiriki michuano ya CAF Women’s Africa Cup of Nations (WAFCON) 2024, itakayofanyika mwaka huu huko Nchini Morocco
#DktSamiamiakamitatuMichezoni
