MV HAPA KAZI TU KUANZA MAJARIBIO WIKI KESHO
MWANZA
Meli mpya ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu iliyojengwa hivi karibuni kwa gharama ya zaiidi ya shilingi bilioni 111 inatarajiwa kuanza majaribio ya awali katika Ziwa Victoria Machi 25 mwaka huu ambayo imejengwa na serikali ya Tanzania kwa kuwatumia wakandarasi kutoka kampuni za za Korea Kusini - Gas Entec kwa kushirikiana na Kangnam Coorporation.
Majaribio ya awali yatahusisha tu wataalam wa ujenzi wa meli, kwa madhumuni ya usalama.
Kampuni za Korea Kusini - Gas Entec kwa kushirikiana na Kangnam Corporation wamepewa kandarasi ya kujenga meli hiyo.
Meli ya Mv Mwanza ndicho chombo cha usafirishaji kwa njia ya maji chenye umbo mkubwa kuliko vyombo vyote Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ikiwa na kimo cha ghorofa nne yenye urefu wa mita 92.6, upana wa mita 17 na uzito wa tani 400 za mizigo na abiria 1,200,pia ndio meli ya kwanza kujengwa ndani ya nchi, mradi pia umeunda wataalam kupitia ujuzi na uhamishaji wa maarifa kutoka kwa wageni kwenda kwa wazawa.
