TANZANIA MWENYEJI WA KONGAMANO EAPCE'25
DAR ES SALAAM
Tanzania itaonesha tena uwezo wake wa uwekezaji itakapokuwa mwenyeji wa Kongamano na Maonesho ya 11 ya Petroli ya Afrika Mashariki (11th East African Petroleum Conference and Exhibition 2025 -EAPCE’25) mwaka 2025
Kongamano hilo litakaloandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), litafanyika kuanzia Machi 5 hadi 7 mwaka 2025 ambalo linatarajiwa kuvutia zaidi ya wajumbe 1,000, linalenga kuangazia fursa za mafuta na uwekezaji katika eneo hili.
Katika miongo miwili iliyopita, makongamano ya kila baada ya miaka miwili ya EA petroli yametumika kama majukwaa muhimu ya mazungumzo kati ya serikali na wahusika wa sekta kuhusu unyonyaji wa rasilimali za hidrokaboni.
EAC inaona mikutano hiyo inaendana na Dira yake ya 2050 ya uwekezaji wa mafuta ya petroli kwa usambazaji endelevu wa rasilimali za nishati.
Dira ya EAC 2050 inatazamia mchanganyiko endelevu, nafuu na salama wa nishati ili kukidhi mahitaji ya kikanda, hasa katika ufikiaji na uhifadhi, Aidha tangu kuanzishwa kwake, Mikutano ya Petroli ya Afrika Mashariki imekuza uelewa wa uwezo wa petroli wa kanda na maendeleo ya kiteknolojia.
