MIAKA MITATU YA DKT SAMIA MBINGA WAPOKEA TSH BIL 11+ ZA MIRADI
RUVUMA
Katika kipindi cha takriban miaka mitatu ya utawala wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, (Machi 2021-Machi 2024) serikali ya awamu ya sita imetoa jumla ya shilingi bilioni 11.97 kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma
kiasi hicho kimetekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya sekta za Elimu, Afya, Maendeleo ya Jamii, Kilimo, Mifugo, Utawala na Biashara.
Mchanganuo wa fedha hizo ni kama ifuatavyo katika mwaka wa fedha 2021/22, Halmashauri ya Mji wa Mbinga ilipokea jumla ya shilingi bilioni 5.6, katika miaka iliyofuata (2022/23 na 2023/24 , ilipokea shilingi bilioni 5.4 na shilingi milioni 974 mtawalia.
Aidha Kwa kutambua ukweli kwamba elimu ni ufunguo wa mafanikio, katika kipindi cha karibu miaka mitatu, sekta ya elimu ilipata msukumo wa shilingi bilioni 7.8 kutoka serikalini.
Miradi iliyotekelezwa katika kipindi cha rejea ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa 182, shule nne mpya ambazo ni Lusonga Sekondari, Dk Philip I. Mpango Sekondari, Matengo Msingi na Mpepai Msingi.
