DKT SAMIA AMEFANYA MENGI MKOANI TANGA
TANGA
Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuboresha huduma za kijamii nchini, ameendelea na jitihada za kuhakikisha ustawi wa wananchi unakuwa kipaumbele, kwa kuhakikisha hilo kwa vitendo Dkt Samia kwa Mkoa wa Tanga amepeleka miradi mingi ya maendeleo ili kuwagusa wananchi hao.
Kwa upande wa Sekta ya Afya, Jiji la Tanga lina vituo Sita vya Afya ambavyo vinafanya kazi, serikali imesambaza mashine za kisasa za uchunguzi ikiwemo CT-Scan katika hospitali ya Rufaa ya Bombo Tanga Mkoani humo
FAIDA:- Kwa uwekezaji huu wananchi wa Mkoa wa Tanga sasa hivi hawana haja ya kwenda tena Dar Es Salaam au Kilimanjaro kwa ajili ya kufuata huduma za CT-Scan au huduma za kusafisha damu, huduma zote hizo zinapatikana Mkoani hapo.
