TANZANIA KUTUMIA DIJITALI NDANI YA MAHAKAMA
ZANZIBAR
Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza jukumu muhimu la teknolojia katika kukuza haki na maendeleo wakati wa hotuba yake kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Sheria wa Jumuiya ya Madola unaoendelea Zanzibar kuanzia Machi 4 hadi 8 mwaka huu
Kupitia hotuba yake aliyoitoa siku ya ufunguzi wa mkutano huo Dkt Samia amesema dhamira ya Tanzania ni kutumia mfumo wa kidijitali ndani ya mahakama ili kutatua changamoto na kuboresha upatikanaji wa haki.
“Juhudi za mahakama ya Tanzania kukabiliana na mrundikano wa kesi kupitia upitishaji wa zana za kielektroniki, vikao vya mahakama vya mtandaoni, mifumo ya kufungua jalada kielektroniki, na akili bandia. Hatua hizi zinalenga kuimarisha uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika mfumo wa sheria” Amesema Mhe Samia.
ZINGATIA:- kupitia ripoti ya Tume ya Haki Jinai Tanzania Julai 2023 Serikali ya awamu ya sita imejipambanua wazi kuboresha mfumo wa haki za jinai, kukuza haki, ufanisi, na kuzingatia haki za binadamu, hivi vimekuwa vipaumbele katika sera ya mahakama ya Tanzania.
