DKT SAMIA AZUNGUMZA NA WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA ABIY AHMED

 

DKT SAMIA AZUNGUMZA  NA WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA  ABIY AHMED

DKT SAMIA AZUNGUMZA  NA WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA  ABIY AHMED

DAR ES SALAAM.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed Ikulu jijini Dar es Salaam leo, ambapo Viongozi hao wawili wameshuhudia kutiwa saini kwa mikataba kadhaa ya maelewano yenye lengo la kuimarisha uhusiano wa kibiashara zikiwemo kilimo, nishati biashara na ushirikiano wa kitamaduni.
baina ya nchi zao.
Kupitia ukurasa wa Twitter (X) wa waziri mkuu wa Ethiopia  ameandika "Mkutano wa leo wa baina ya nchi mbili ni ushuhuda wa jinsi uhusiano wetu wa kihistoria umefungua njia ya uhusiano wenye nguvu zaidi kwa sasa," 
Aidha Mh Abiy ametoa pole kwa Tanzania kwa kuondokewa na aliyekuwa Rais wa pili wa Tanzania Haati Ali Hassan Mwinyi
"Kwa niaba ya Ethiopia, natoa pole kwa kuondokewa na aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Ali Hassan Mwinyi," Ahmed amesema.

#PumzikaKwaAmaniMzeeMwinyi