MHE.RAIS SAMIA ATOA PONGEZI KWA KLABU YA SIMBA
ZANZIBAR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa pongezi kwa klabu ya Simba kwa kufanikiwa kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kupata ushindi wa goli 6-0 dhidi ya Jwaneng Galaxy
Pongezi hizo amezitoa kupitia kurasa za mitandao yake ya kijamii (Instagram &Twitter) kwa kuandika
"Hongereni sana Klabu ya Simba kwa kufanikiwa kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mafanikio yenu si tu furaha na fahari kwa mashabiki na wanachama wa Klabu ya Simba, bali pia kwa Taifa na Watanzania wote"
Bimkubwatanzania tunaungana na Mhe Rais Dkt Samia kuipongeza Klabu ya Simba kwa kufuzu hatua ya robo fainali Ligi ya mabingwa Afrika.
