DKT SAMIA AHANI KWA WAZIRI MASAUNI
ZANZIBAR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Machi 3, 2024 ameshiriki dua ya pamoja na familia ya Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Hamad Masauni kwa ajili ya kuhani kufuatia kifo cha Baba yake Mzee Masauni Yussuf Masauni aliyefariki dunia tarehe 23 Februari, 2024.
