MAZINGIRA RAFIKI YA UWEKEZAJI, YAKUZA KILIMO-BOT

 

MAZINGIRA RAFIKI YA UWEKEZAJI, YAKUZA KILIMO-BOT

MAZINGIRA RAFIKI YA UWEKEZAJI, YAKUZA KILIMO-BOT

DAR ES SALAAM
Sekta ya kilimo inaongoza katika orodha ya sekta zinazovutia ukuaji wa juu wa mikopo kutokana na kuboreshwa kwa mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.
Ripoti ya hivi karibuni ya mapitio ya uchumi ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya mwezi Januari 2024 inaonesha kuwa mikopo iliyotolewa kupitia kilimo imefikia asilimia 43.5 ikilinganishwa na asilimia 38.9 katika kipindi kilichopita.
Ukuaji mkubwa wa mikopo kwenye kilimo unachangiwa na hatua kadhaa zinazolenga kuweka mazingira rafiki kwa sekta hiyo kuweza kujiendesha kibiashara kwa wakopeshaji kutoa mikopo.
Kwa mfano, moja ya hatua ilikuwa BoT kupunguza kiwango cha chini cha akiba kisheria (SMR) ambacho ni sawa na mkopo unaotolewa na benki inayotoa mikopo kwenye sekta ya kilimo.
Kwa mujibu wa BoT, benki inatakiwa kuwasilisha ushahidi wa mikopo kwa kilimo kwa riba isiyozidi asilimia 10 kwa mwaka.
Hatua hii na hatua nyingine za serikali zimechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza ukuaji wa mikopo kwenye sekta ya kilimo.
Sekta ya Kilimo nchini inaajiri takribani 70%  ya nguvu kazi ya Watanzania na inachangia karibu 26%  ya Pato la Taifa