MANISPAA YA SINGIDA BARABARA ZIPO SAFI

 

MANISPAA YA SINGIDA BARABARA ZIPO SAFI

MANISPAA YA SINGIDA BARABARA ZIPO SAFI

SINGIDA
Utekelezaji wa miradi ya barabara katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida upo katika hali nzuri kwa 75% na Manispaa hiyo ina jumla ya mtandao wa barabara wenye urefu wa Km 523.
Aidha serikali kupitia TARURA  kwa sasa inatekeleza  miradi miwili ya ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami eneo la Mnung’una na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami eneo la Mwenge-Mungumaji ambapo kaisi cha shilingi bilioni 2.7 kimetengwa.
Chanzo:-Meneja  wa TARURA Mkoa wa Singida, Eng. Ibrahimu Kibasa 
Serikali kupitia TARURA itaendelea  kuboresha barabara za Manispaa na Halmashauri nyinginezo kwa kuhakikisha zinakuwa katika ubora kwa kiwango cha lami, changarawe na kujenga madaraja katika maeneo mbalimbali yaliyo na changamoto.