BANDARI YA TANGA YAPOKEA SHEHENA ZA SULPHUR

 

BANDARI  YA TANGA YAPOKEA SHEHENA ZA SULPHUR

BANDARI  YA TANGA YAPOKEA SHEHENA ZA SULPHUR

TANGA
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Bandari ya Tanga imepokea shehena ya mzigo wa Sulphur tani 27,001 iliyoletwa na meli ya Kharis Trinity yenye urefu wa mita 189.9 kutoka Kuwait.
 Hatua hiyo imekuja baada ya maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita  kwa ajili ya kuijengea uwezo Bandari ya Tanga ili iweze kupokea shehena zaidi na meli kubwa gatini.
Ujio wa meli hiyo umezidi kuleta chachu ya maendeleo  kwa Mkoa wa Tanga na Taifa kwa ujumla, hatu hii ni baada ya wafanyabiashara wa Kanda ya Kaskazini na nchi jirani kuchagua kuitumia Bandari ya Tanga